Zamaradi sasa aja kivingine
MTANGAZAJI Zamaradi Mketema amezindua rasmi Chaneli yake ya Zamaradi Tv ambayo itapatika katika kingamuzi cha azam Tv cha dishi katika chaneli namba 413.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo, jijini dar es salaam amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu na shughuli nyingi zilisimama katika kuhakikisha ndoto ya kuzindua tv inakamilika.
“Sababu ya kubwa ya kuchelewa ni kwamba tulizindua online tv na tukatangaza kuwa tutazindua tv na tulitamani jambo hili lisiwe na mkono wa mtu tusimamie sisi wenyewe”amesema Zamaradi.
Ameongeza kuwa fundisho kubwa alilolipata katika ndoto yake ni hakuna kitu kwa kwaajili ya mtu fulani kila kitu ni kwa kila mtu.
“Ningeweza kukata tamaa na kuona kuwa hii ni ya watu fulani lakini nimepiga na kuhakikisha nimefika hapa nilipofika leo, maneno ni mengi ya kukatisha tamaa na kama unaroho ndogo unaweza kukata tamaa kutimiza ndoto yako” amesema zamaradi.
Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Azam tv, Gloria Chuwa amesema wanafuraha kubwa kuweza kutambulisha ushirikiano baina ya Azam tv na zamaradi tv.