Zambia yakumbwa na ukame

RAIS wa Zambia, Hakainde Hichilema ametangaza hali ya dharura ya janga la kitaifa la ukame wa muda mrefu unaoendelea kuathiri taifa hilo.

Kiongozi huyo amesema wilaya 84 kati ya 116 zimeathirika na ukame.

Zambia imekuwa na mvua chache, huku hofu ikiwa pengine nchi hiyo huenda ikakumbwa na njaa na changamoto ya nishati ya umeme.

Imeelezwa viwango vya maji katika Bwawa la Kariba vilipungua hadi asilimia 11.5 ya hifadhi inayoweza kutumika kufikia Desemba mwaka jana.

Hichilema alisema ukame huo utaathrii uzalishaji wa zaidi ya megawati 450 za nishati hiyo.

Alisema karibia nusu ya ardhi inayotumika kupanda mimea imethiriwa na kiangazi, na kuongeza kuwa serikali itajitahidi kuhakikisha mahindi na vyakula vingine vinaletwa kufidia upungufu uliopo

Habari Zifananazo

Back to top button