Zamu ya vijana uongozi Serikali za Mitaa

NYAMAGANA, Mwanza: VIJANA wameshauriwa kuchukua fomu na kugombea nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu.

Wito huo umetolewa leo na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana, Omary Ramadhani wakati wa maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika katika shule ya sekondari Mtoni katika kata ya Mabatini mkoani Mwanza.

‘’Vijana bado tunayo nafasi kubwa sana katika kugombea nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa nakupitia nafasi hizo tunaweza kusaidia jamii katika mambo mbali mbali,’’ amesema.

Ramadhani amewaomba viongozi mbalimbali wa chama chao kuwa tayari kuwasaidia vijana katika ushauri na mawazo kwa vijana wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake nchini (UWT) Wilaya ya Nyamagana, Witnes Makale amewashuari pia vijana na wanawake wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kugombea nafasi za wenyeviti na wajumbe.

Amesema Wilaya ya Nyamagana kuna mitaa 175 na yote inaongozwa na wenyeviti kutoka CCM.

Habari Zifananazo

Back to top button