Zenji patawaka leo

ZANZIBAR: Wakazi wa Zanzibar leo watashuhudia mtanange wa kirafiki kati Zanzibar Hereos na Kilimanjaro Stars.
Shauku ni kubwa kwa wapenda soka Tanzania kutokana na mchezo huo kuwakutanisha wachezaji wengi wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars lakini leo watakuwa timu pinzani kupambana ndani ya Uwanja wa Amaan.
Mchezo huo maalumu ni kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Amaan baada ya kufanyiwa ukarabati na kuwa na muonekano mpya wa kisasa.
Moja ya maeneo yanayotizamwa zaidi katika mchezo huo ni upinzani katika eneo la kiungo
 
Ambapo kwa upande wa Zanzibar Hereos eneo la kiungo linatarajiwa kuongozwa na nahodha wa kikosi hicho Feisal Salum pamoja na Mudathir Yahya wakati kiungo cha Kilimanjaro Stars kikitarajiwa kumilikiwa na Mzamiru Yassin na Sospeter Bajana ama Yusuph Kagoma.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 2:15 usiku ukitanguliwa na sherehe za uzinduzi , mgeni rasmi atakua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.

Habari Zifananazo

Back to top button