Zari atoa neno kwa Zuchu

DAR ES SALAAM; Zari Hassan ambaye ni mzazi mwenza wa msanii, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amempa sifa msanii Zuhura Othman ‘Zuchu’ kwamba ni mlezi mzuri wa familia na ana tabia nzuri.

Zari raia wa Uganda anayeishi Afrika Kusini, ametoa kauli hiyo leo katika mkutano na wana habari baada ya kuulizwa swali kama anajisikiaje watoto wake wakija Tanzania wanavyolelewa na mwanamke mwingine.

Akizungumza katika mkutano wake kueleezea kuhusu kuongeza mkataba wa kutangaza bidhaa za kampuni ya Softcare, Zari amesema watoto wake wakija Tanzania wanapata malezi kutoka kwa Zuchu ambaye ni mwenza wa Diamond kwa sasa, hivyo binafsi anakuwa na amani sana kwamba wapo katika mikono sahihi na wanafurahi kuwa naye na wanampenda.

Pia Zari amesema anazungumza vizuri na familia ya Diamond kuanzia mama yake na ndugu zake wengine, huku akisisitiza kuwa watoto wake wakiwa Tanzania huwa anampigia simu Zuchu kuzungumza nao.

Habari Zifananazo

Back to top button