Zelensky: Asanteni kwa vifaru
Rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky amewashukuru viongozi wa nchi Magharibi kwa kuwapa msaada wa vifaru kwa ajili ya kupambana na Urusi na kuongeza kuwa wanatakiwa kuvituma haraza iwezekanavyo.
Katika hotuba yake ya usiku, Zelensky amekubali kupokea msaada wa makombora ya masafa marefu, na ndege za kivita. Rais huyo amezungumza hayo badaa ya Marekani na Ujerumani jana kukubali kuwapa Ukraine vifaru vya vita.
Aidha, Urusi imelaani hatua hiyo na kuiita “uchochezi wa wazi” na kusema kuwa vifaru vyovyote vilivyotolewa watavisambaratisha.
Mizinga hiyo “itawaka kama wengine wote,” alisema Dmitry Peskov, msemaji wa Rais Vladimir Putin.
Zelensky alisema alimwambia Katibu Mkuu wa Nato, Jens Stoltenberg kwamba “maendeleo lazima yafanywe katika nyanja nyingine za ushirikiano wa ulinzi huku Ukraine ikitafuta ugavi wa makombora ya masafa marefu na mizinga.
Alisisitiza kuwa sio tu kuwasilishwa haraka kwa mizinga hiyo, lakini pia kwa idadi kubwa.