Zelensky: Tukishinda tutafanya uchaguzi

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema nchi hiyo haitofanya uchaguzi Mkuu 2024 hadi hapo watakapoishinda Urusi katika vita inayoendelea baina ya nchi hizo mbili na nchi washirika.

Taarifa hiyo ameitoa wakati akijibu swali katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC mwishoni mwa juma lililouliza iwapo nchi hiyo itashiriki katika uchaguzi Mkuu mwakani.

“Uchaguzi wowote ni lazima ufanyike kipindi cha amani, kipindi hakuna vita na hii ni kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Advertisement

Itakumbukwa, Rais Zelensky aliingia madarakani kwa kushinda uchaguzi mkuu wa taifa hilo Aprili 2019 kwa asilimia 73 dhidi ya Rais aliyekuwa akimaliza muda wake Petro Poroshenko aliyepata asilimia 24 ya kura.

Hata hivyo Urais wa Zelenskyy unatarajiwa kufikia ukomo mwishoni mwa mwaka 2023 kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo.

1 comments

Comments are closed.