Zelenskyy aiwakia Urusi

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amelaani mashambulizi makali yanayofanywa na jeshi Urusi dhidi ya taifa hilo kwa kuyaita ni mashambulizi ya kigaidi

Zelenskyy amesema hayo kupitia hotuba yake kwa njia ya vidio na kuyataja maeneo yaliyoathirika zaidi kuwa ni Odessa, Chornomorski, na bandari kadhaa za nchi hiyo

“Pengine hili ni jaribio kubwa zaidi kufanywa na Urusi ili kutusababishia maumivu katika eneo la Odessa kwa kipindi chote cha vita inayoendelea.”

Advertisement

Aidha, Zelenskyy amelishukuru jeshi la anga la  nchi hiyo kwa kusema mashambulizi yaliyodhibitiwa ni makubwa hivyo kupunguza madhara yaliyotakiwa kutokea.

Hata hivyo, mashambulizi haya ya Urusi ni ulipaji wa kisasi kufuatia mwanzoni mwa juma kuripotiwa kulipuliwa daraja la Kerch, lililopo Jamhuri ya Crimea inayounda Shirikisho la Urusi.

Itakumbukwa ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi 10 ya hivi karibuni daraja la Kerch limelipuliwa, ingawa hakuna kundi lililojitokeza kukiri kuhusika na mlipuko huo.

7 comments

Comments are closed.