Zelenskyy aomba msaada wa kijeshi Ujerumani 

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amewasili na kupokelewa na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini humo tangu kuanza kwa vita ya Urusi ya Ukraine.

Zelenskyy amewasili nchini humo kuomba msaada wa jeshi kwa ajili ya kuisaidia nchi yake kukabiliana na Urusi pamoja na msaada wa kifedha kwa ajili ya kutengeneza upya maeneo na mali zilizoteketea kwa takribani mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita hivyo.

Kabla ya kuwasili Ujerumani, rais huyo alifika Rome nchini Italia na kukutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Pope Francis pamoja na Waziri Mkuu, Giorgia Meloni jana Mei 13, 2023.

Serikali ya Ujerumani ilitangaza hatua mpya ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine wenye thamani ya zaidi ya Euro bilioni 2.7  ikiwa ni pamoja na vifaru, mifumo ya kupambana na ndege na risasi.

“Tayari huku Berlin, silaha na kifurushi vyenye nguvu, ulinzi wa anga ujenzi upya EU NATO Usalama,” Zelenskyy ametweet leo, katika kumbukumbu dhahiri ya vipaumbele muhimu vya safari yake.

Habari Zifananazo

Back to top button