Zelothe kuzikwa kijijini kwake Jumatatu

ARUSHA: MWILI wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Arusha, Zelothe Stephen aliyefariki Dar es Salaam jana, utazikwa Jumatatu Oktoba 30,2023 kijijini kwake Olosiva Kata ya Olorieni wilayani Arumeru.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulani Ramsey amesema mwili huo utawasili kwa ndege Arusha kesho ukitokea Dar es Salaam.

Amewaomba wananchi kujitokeza alasiri kuupokea mwili huo Uwanja wa Ndege wa Arusha uliopo Kisongo.

“Nitoe pole kwa wananchi wa mkoa huu kufuatia msiba huo, lakini pia niwaombe tujitokeze kuupokea mwili wa baba na kiongozi wetu ambaye alituongoza kwa upendo na kuhimiza mshikamano na umoja ili kuonesha mapenzi yetu kwake,” amesema.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button