Ziara ya Chongolo Mufindi, Kiwanda cha Parachichi kujengwa

KIWANDA cha Parachichi kipo mbioni kujengwa katika Kata ya Nyororo Mufindi Kusini mkoani Iringa.

Hayo yamesemwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ambae aliwataka wananchi wa Nyororo kuchangamkia fursa za biashara ili kuinua vipato vyao.

Katika ziara hiyo, Chongolo alimpongeza Mbunge wa Mufindi Kusini David Kihenzile kwa kuhakikisha mchakato wa ujenzi wa Kiwanda hicho unafanikiwa.

Aidha, Chongolo ameelekeza vijiji vya Njonjo, Luwing’ato na Nyororo shuleni vifikishiwe maji haraka na kuagiza mkandarasi atafutwe haraka.

Pia, ameahidi kuziwasilisha bati 100 kwa katika Kituo cha afya ikiwa ni ahadi iliyotolewa na CCM mwaka 2014.

Wakati huo huo Mbunge wa Mufindi Kihenzile kwa niaba ya wananchi wa Mufindi ametoa ng’ombe kwa Rais Samia Suluhu Hassan, pia ametoa mbuzi kwa wasimamizi wa idara mbali mbali za CCM na kuku Kwa watumishi wa CCM Makao Makuu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button