ZIC yapewa tuzo huduma bora

DAR ES SALAAM; SHIRIKA la Bima Zanzibar (ZIC) limeshinda tuzo iitwayo ‘Africa Outstanding Award’ kwa kuwa shirika linalotoa huduma bora za bima Afrika.

ZIC ilipata tuzo hiyo jana, katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pia watu mbalimbali wanaowakilisha taasisi na kampuni kutoka Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ghana walishiriki.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZIC,upitia Mkurugenzi wake mwezeshaji Arafati Haji,  mwakilishi wa shirika hilo, Muhammad Said Matumula amesema tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na shirika.

“Kwa niaba yake nimefurahi sana kwa sababu mafaniko ya yeye aliyekuwa mbele ni mafaniko ya sisi tuliopo nyuma yake, hii tuzo sio ya Tanzania peke yake,” amesema Matumula.

Matumula amesema tuzo hiyo itakuwa sababu ya kuwapa nguvu na chachu ya kupambana ili kuhakikisha tuzo zingine wanazipata kutokana na utendaji kazi wao mzuri.

“Kama hizi tuzo zinatolewa kwa kufuata huduma bora, basi naamini tutazichukua nyingi sana,” ameongeza Matumula.

Tuzo za Tatu za Wataalamu Bora wa Kiafrika ni mpango wa tuzo za bara zima iliyoundwa na kutambua wataalamu wenye uwezo na waliokamilika katika nyanja mbalimbali za shughuli zao.

Advertisement