ZIMBABWE imetangaza hali ya dharura katika mji Mkuu wa Harare kufuatia mlipuko wa Kipindupindu.
–
Mlipuko huo hadi sasa umeua makumi ya watu huku kukiwa na kesi 7,000 zinazoshukiwa.
–
Wakuu wa jiji wanasema mlipuko huo, unaoenea katika jiji lote, umeibua kumbukumbu za mlipuko mbaya mnamo 2008, ambapo maelfu walikufa.
“Tumetangaza hali ya hatari kwa sababu ya kipindupindu,” Meya Ian Makone alisema.
Mamlaka sasa inaomba msaada wa kudhibiti kuenea na kutoa maji salama, ikisema msaada unaopokelewa hautoshi.
Mamlaka za afya zimekuwa zikijitahidi kudhibiti idadi kubwa ya waliolazwa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo.
Comments are closed.