Zimbwe ajivunia kinyang’anyiro beki bora

MLINZI wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein “Tshabalala’ amesema ni fahari kwake kujumuishwa kwenye kivumbi cha kuwania tuzo ya beki bora wa msimu wa Ligi Kuu Bara.

Tshabalala anasema siku zote anapokuwa uwanjani malengo yake ni kuisaidia timu yake lakini pia kuonesha ubora wake hivyo anapojumuishwa kwenye kinyang’anyiro kama hicho huwa ni fahari kubwa kwake.

“Kwangu ni jambo kubwa, siku zote wanasema ukifanya jambo kwa bidii au kwa nguvu kubwa huwa inaonekana, niwapongeze wachezaji wenzangu wa simba Inonga, na Kapombe walio pia katika tuzo hii yeyote atakaechukua nitajiskia fahari”Alisema Mohamed Hussein.

Wachezaji wengine wanawania tuzo hiyo ni walinzi wa Yanga Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

Habari Zifananazo

Back to top button