Zitto ataka masoko ya wakimbizi kuimarisha uchumi

KIGOMA; Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka idara ya wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kurudisha masoko ya pamoja baina ya wananchi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma na wakimbizi wa Burundi katika Kambi ya Nduta wilayani Kibondo ili kuimarisha uchumi wa wananachi wa wilaya hiyo.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Kibondo akiwa kwenye mfululizo wa ziara ya mikutano yake mkoani Kigoma katika kuimarisha chama hicho kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025 amesema kuwa masoko hayo ni muhimu katika kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.

Ameomngeza sehemu kubwa ya wananchi hao ni wakulima na wanafanya biashara yao hivyo kuwepo kwa masoko hayo kunawapa nafasi kubwa ya kufanya biashara na kuimarisha hali zao za uchumi.

Sambamba na hilo Zitto amekemea tabia ya Polisi na maofisa uhamiaji mkoani Kigoma kutumia vizuizi vinavyowekwa barabarani katika maeneo mbalimbali ya barabara za Mkoa wa Kigoma kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao badala ya vizuizi hivyo kutumika kutesa na kunyanyasa wananchi.

Awali Akizungumza katika mkutano huo Naibu Waziri kivuli viwanda na biashara wa chama cha ACT Wazalendo, Julius Masabo alisema kuwa bado hali za wananchi wa Wilaya Kibondo kiuchumi ni mbaya kutokana na kutokuwepo kwa jambo kubwa la kiuchumi ambalo wanaweza kulitumia kuimarisha hali zao hivyo uwepo wa masoko ya pamoja baina ya wananchi hao na wakimbizi yalikuwa na faida kubwa kiuchumi kwa wananchi.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button