MAZUNGUMZO kati ya Hakim Ziyech na Al-Nassr juu ya mpango wa kiungo huyo wa Chelsea kujiunga na klabu hiyo kutoka Saudia Arabia yanaendelea kuleta matumaini.
Imeelezwa na Fabrizio Romano kuwa Chelsea inapambana kukamilisha uhamisho huo. Ziyech yuko tayari kujiunga na timu hiyo anayochezea Cristiano Ronaldo.
Kiungo huyo raia wa Morocco alijiunga na Chelsea 2020 akitokea Ajax ya Uholanzi.
24 Feb 2020 alisaini mkataba wa miaka mitano na mpaka sasa amebakisha miaka miwili pekee kwenye mkataba wake.