Trending

Zoezi la Sensa Mtwara linaendelea usiku wa manane

ZOEZI la Sensa ya Watu na Makazi 2022 limeanza saa 6:01 leo Agosti 23 katika kiwanda cha Saruji cha Dangote wilayani Mtwara mkoani Mtwara na linaendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dustan Kyobya akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya, Thomas Salasala wamefika katika kiwanda hicho kuhakikisha wafanyakazi zaidi 3000 wa kiwanda hicho wanahesabiwa ipasavyo.

“Kiwanda Cha Dangote ni kiwanda muhimu na kikubwa ambacho kimeajiri wafanyakazi zaidi ya 3000 na kwa sababu hiyo tumeiona ni muhimu kufika na kuhakikisha kuwa zoezi linaenda vizuri,” amesema.

Baada ya kufika Kyobya alikuta zoezi hilo linaendelea vizuri ambapo makarani tayari wapo wanaendelea kuhesabu wafanyakazi hao, wengi wao wakiwa wakipakia Saruji kwa ajili ya kusafirisha kwenda sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa hatua nyingine Kyobya amesema zoezi hilo pia linaendelea katika maeneo mengine Kama vile  hospitalini, nyumba za kulala wageni vituo vya mabasi na daladala. Kuhusu usalama Kyobya amesema hali ni shwari na kwamba serikali ya Mkoa na Wilaya imejipanga vizuri kuhakikisha usalama unaendelea kuwepo .

Habari Zifananazo

Back to top button