ZRB yavuka malengo ukusanyaji wa mapato

Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) imevuka malego yake ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka huu wa fedha kuanzia Julai hadi Novemba 2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amesema bodi hiyo imekusanya Shilingi bilioni 236.39 ikiwa lengo ilikua ni kukusanya bilioni 238.5 na kupelekea kufikia asilimia 99.1 ya ufanisi wa makusanyo hayo.

Akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mwezi wa shukrani na furaha kwa walipakodi, Dk Mwinyi amesema kwa kiasi kikubwa malengo hayo yamefanikiwa kutokana na ufanisi mzuri wa kasi ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.

Dk Mwinyi ameipongeza bodi hiyo kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato.

Aidha, Waziri wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dk Saada Mkuya Salum amesema kwa kushirikiana na watendaji wa bodi kuhakikisha makusanyo ya kodi yanaongezeka na kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button