ZSTC kutumia jengo la Karafuu House

RAIS Samia suluhu Hassan amelitaka Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar (ZSTC) kulitumia kibiashara jengo la kitega uchumi la shirika hilo maarufu kama Karafuu House kibiashara ili kuleta tija katika ujenzi wake.

Rais Samia ameyasema hayo  leo alipozungumza na wananchi visiwani Zanzibar kabla ya uzinduzi wa jengo la Kitega Uchumi la Zanzibar State Trade Cooperation – Pemba visiwani Zanzibar.

“Rai yangu kwenu, au kwa wizara au kwa shirika ZSTC kuhakikisha kuwa jengo hili linatumika ipasavyo ili lifikie malengo yake katika kuendeleza zao hili (Karafuu)”.

“Lakini imesemwa hapa jengo hili ni kitega uchumi, ni matumaini yangu kuwa shirika mtalitumia jengo hili vyema, kutafuta fedha ambazo haitalazimisha sasa hazina ya serikali kutoa fedha kuwapa shirika” aliongeza.

Habari Zifananazo

Back to top button