Zuchu afungiwa miezi sita

Zuchu

BARAZA la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa Zuhura Othman, ‘Zuchu’ kuendesha shughuli za sanaa visiwani Zanzibar kwa muda wa miezi sita na faini ya Sh million 1.

Kifungo hicho kimetokana na onesho lake la Februari 24 mwaka huu ambapo alitoa maneno yenye ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili.

Zuchu kafungia kuendesha kufanya shughuli za sanaa, wamepiga marufuku kazi zake kupiga kwenye redio na televisheni za Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita.

Advertisement

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024,” amesema.