Zuchu: Mimi na Diamond basi
ZANZIBAR: Msanii wa Bongo fleva ,Zuhura Othumani Zuchu ametangaza rasmi kuachana na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zuchu ameandika kuwa wameachana kwa sababu hakuna heshima aliyotamani kuipata.
“Hello fan Milly I had to post this to clear my Conscience kuanzia leo hii mimi na Naseeb (Diamond) hatuko pamoja. I know this has been our thing but its hard kumuacha mtu unaempenda hii naomba Mungu iwe ya mwisho na nianze maisha mapya. Ameandika msanii huyo na kuongeza..
” Tumeishi vizuri lakini nadhani hii sio riziki.”
“Mwaka huu nimejifunza kusema hapana kwa kila kitu kisichonipa furaha na baada ya kusema haya naona kabisa naenda kuanza maisha ya furaha naona kabisa naenda kuanza ukurasa mpya wenye furaha, uhuru, amani na as for nows kazi iendelee and am single amemalizia Zuchu.