Zuchu: Sichoti fedha za Diamond

Zuchu

MSANII wa Bongo Fleva nchini, Zuhura Othuman ‘Zuchu’ amesema matumizi mbalimbali anayofanya anatumia fedha zake na wala sio fedha za bosi wake Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Amesema licha ya kazi ya usanii ambayo inampatia fedha za kutosha, lakini pia amekuwa balozi wa taasisi na kampuni mbalimbali, kazi ambazo zinampatia pia fedha, hivyo isionekane kwamba Diamond ndiye anampa fedha.

“Sio kweli kwamba nachota pesa za Diamond Platnumz kama mnavyosema jamani, nafanya kazi, napata pesa zangu, si mnaona ninavyoachia kazi,  mashabiki ni mashahidi, kazi zangu  ndizo zinazonilipa na ubalozi nilionao,”amesema Zuchu.

Advertisement