Zuma akata rufaa marufuku ya uchaguzi

AFRIKA KUSINI; Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amewasilisha rufaa dhidi ya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, ambayo wiki iliyopita ilimzuia kugombea katika uchaguzi ujao.

Zuma ,81, alihudumu kama rais kuanzia 2009 hadi 2018, ambapo alilazimika kujiuzulu kwa madai ya ufisadi.

Alipatikana na hatia na akapata kifungo cha miezi 15 jela mwaka 2021 kwa kudharau mahakama na katiba inasema mtu yeyote ambaye amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 hastahili kugombea.

Shirika la habari la AFP linaripoti kwamba karatasi zilizowasilishwa mahakamani kwa niaba yake zinasema kwamba tume ya uchaguzi ”haikuwa na sababu halali za kukiuka haki za kisiasa za Zuma”.

Habari Zifananazo

Back to top button