Zumaridi ana kesi ya kujibu, kuanza kujitetea Oktoba 17

Zumaridi ana kesi ya kujibu, kuanza kujitetea Oktoba 17

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoani Mwanza imesema kiongozi wa kidini, Diana Bundala maarufu kwa jina na Mfalme Zumaridi na wenzake wanane wana kesi ya kujibu katika kesi ya kumshambulia na kumsababishia madhara ofisa wa serikali.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Monica Ndyekobora alisema jana Zumaridi na wenzake wamekutwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa serikali kuwasilisha ushahidi dhidi yao.

Ndyekobora aliagiza upande wa utetezi ujiandae kuanza kujitetea kuanzia Oktoba 17 hadi 21 mwezi huu.

Advertisement

Wakili wa Mfalme Zumaridi, Erick Muta alisema watakuwa na mashahidi 30 na vielelezo 12.

Katika kesi hiyo namba 10 ya mwaka huu, Zumaridi na wenzake wanakabiliwa na mashitaka likiwemo la kuwazuia maofisa wa Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yao walipoenda kwenye makazi ya kiongozi huyo wa kiroho.Wanadaiwa pia kusafirisha na kutumikisha watoto.