DODOMA: NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Hassan Zungu amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ametekeleza miradi ya maendeleo kwa muda mfupi kutokana na kasi ya kiongozi huyo.
Amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mtandao wa Vijana wa Taifa letu kesho yetu, ambapo amesema ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia amegusa kila sekta.
” Mambo makubwa yamefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa miaka mitatu ametekeleza mambo mengi utadhani yuko madarakani miaka 10,” amesema Zungu na kuongeza
“Rais Samia ni Rais wa kwanza Afrika kuthubutu kuunda Tume ya Jaji mstaafu Mohamed Chande kwa ajili ya kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini na tume imezunguka nchi nzima na kuwasikiliza wananchi ikiwemo wale wanaoonewa,” amesema
Pia amewataka vijana kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili washiriki kikamilifu kwenye chaguzi zijazo.