Zungu atahadharisha matumizi ya kuni, mkaa
NAIBU Spika wa Bunge, Azan Zungu amesema mtu anayepikia kuni na mkaa kwa siku ni sawa na mtu anayevuta sigara 300.
Zungu ameyabainisha hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akigawa mitungi ya gesi ya kupikia 40 kwa mama na baba lishe katika soko la Machinga Complex.
Ugawaji wa mitungi hiyo ni sehemu ya mitungi 200 iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa masoko ya Machinga Complex, Karume, Ilala na Mchikichini.
Amesema Rais ametoa mitungi hiyo ikiwa ni hatua ya kupambana na hewa ukaa na kusisitiza matumizi ya nishati safi nchini.
“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa majiko haya ya gesi kwa wananchi wake na hii ni kwaajili ya kulinda afya ya wananchi wake kutokana na matumzi ya mkaa na kuni,”alisema Zungu.
Ameongeza “athari za kutumia mkaa na kuni kwa siku moja ni sawa na kuvuta sigara 300 ambayo ni hatari kwa afya lakini kwa majiko hayo wateja weno watafurahi na watakula chakula cha moto