Zungu: Fanyieni kazi zao la mkonge

NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’ ameitaka serikali kuhakikisha inafanyia kazi suala la kilimo cha zao la mkonge nchini.

Amesema mwaka 1962 Tanzania ilikuwa inazalisha tani 130 ya zao la mkonge, lakini hivi sasa uzalishaji huo hata tani 38,000 haufiki.

Ametoa kauli hiyo baada ya Naibu Waziri wa Viwanda na Bishara, Exaud Kigahe kumaliza kujibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mnzava aliyetaka kujua mkakati wa serikali kuhakikisha bei ya zao la mkonge haitetereki.

“Mheshimiwa Waziri hilo swali la Mnzava la mkonge, mwaka 1962 Tanzania ilikuwa inalima mkonge tani hatufiki hatatani 38,000, hili nendeni mkalifanyie kazi,” amesema Naibu Spika.

Akijibu swali la msingi la Mbunge Mnzava kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri Kigahe amesema katika kuhakikisha bei ya zao la mkonge haitetereki Wizara kupitia Bodi ya Mkonge imechukua hatua mbalimbali.

“Iikiwemo kuimarisha soko la ndani kwa kuongeza matumizi ya ndani katika kutengeneza bidhaa zilizoongezwa thamani kama kamba, mazulia, magunia, mapambo na bidhaa za ufumaji na kupunguza matumizi ya bidhaa za kutoka nje kama uagizaji wa kamba za plastiki, mazulia na vifungashio.

“Mheshimiwa Spika, pia wizara inaendelea kutenga bajeti kila mwaka kuanzia Mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya kununua mashine mpya za uchakataji (Makorona) ili kuhakikisha kuwa ubora wa mkonge unaochakatwa unakidhi matakwa na viwango vya soko la ndani na soko la kimataifa na hivyo kuimarisha bei ya zao hilo,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Tibirizi Chakechake Pemba
Tibirizi Chakechake Pemba
16 days ago

Hela za kujenga ofisi za serikali zimepungua kwa asilimia 100, manager lini tutasini vifone = ajira zitaongezeka kwa asilimia 300

Capture2.JPG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x