Kituo kipya cha mabasi kumaliza msongamano Arusha

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Mkoa wa Arusha, kutapunguza changamoto ya msongamano wa magari katikati ya jiji hilo na kuweka wazi kuwa wajibu wa serikali ni kusimamia mradi huo ukamilike kwa wakati.

Makalla ameyasema hayo leo Julai 29, jijini Arusha wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa kwenye Kata ya Muriet kwa gharama ya Sh bilioni 14.3.
“Stendi hii ni muhimu kwa wakazi wa Arusha, kukamilika kwakwe mwezi Novemba 2026, kunatarajiwa kupunguza foleni katikati ya Jiji pamoja na kurahisisha usafiri na usafirishaji wakati wa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyia mkoani Arusha mwaka 2027,”alisema Makalla.

Awali, RC Makalla amemtaka mkandarasi mzawa anayetekeleza mradi huo M/S Mohammed Bulders LTD, kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati kulingana na mkataba ili wananchi wa Jiji la Arusha wanufaike na mradi huo.



