Wakazi Chilmba waishukuru serikali ujenzi shule mpya

MTWARA: WAKAZI wa kijiji cha Chilimba kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wameishukuru serikali kwa kuwaletea ujenzi wa mradi wa shule mpya ya kisasa unaogharimu zaidi ya Sh milioni 400.

Yamejiri hayo leo Agosti 11, 2026 wakati Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga alipotembea shuleni
hapo kwa lengo la kujionea mradi na kuweka jiwe la msingi.

Aidha, ujenzi huo umekuja baada ya majengo yaliyokuwepo awali shuleni hapo kuwa chakavu kutokana na kuwa ya zamani ambayo yalijengwa mwaka 1930.

Baadhi ya wazazi katika kijiji hicho akiwemo Magreth George amesema kwa sasa watoto wao watasoma kwenye mazingira bora na kuondokana na adha ya kuvujiwa wakati wa mvua.

“Tunafurahi sana kwakweli tunajionea jitihada za serikali kwa kutuona wananchi wa chilimba na kutuletea shule mpya na siku hii ni historia kubwa kwetu,” amesema Magreth

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo Blandina Leonald wa darasa la saba amesema kwa sasa watakuwa na ari ya kupenda kusoma kutokana na mazingira ya kusomea kuwa mazuri.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara Saidi Nyengedi amewataka wananchi wa kijiji hicho kutunza miundombinu hiyo ili isichakae .

Kapinga amewahidi wananchi hao kuwa bado serikali itaendelea kuleta miradi ya maendeleo kwenye kijiji hicho na jimbo hilo la Lulindi kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button