TARI Naliendele yatakiwa kutumia vifaa vipya kwa ufanisi

MTWARA: WATAALAMU wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI)  Naliendele mkoani Mtwara wametakiwa kuendelea kufanya vizuri kazi ya utafiti ili kuleta tija ya uzalishaji kwenye zao hilo.

Akizungumza leo Agosti 13,2026 wakati wa uzinduzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia utafiti na miundombinu  uliyofanyika kwenye Manispaa ya Mtwara Mikindani, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Christopher Magala amesema vifaa hivyo vitumike kwa ufanisi ili kazi hiyo iendelee.

Aidha, vifaa hivyo vilivyozinduliwa ikiwemo pikipiki ishirini, magari mawili, ndege nyuki (Drone) itakayotumika kwenye shughuli ya upuliziaji wa mikorosho na vingine, lengo ni kurahisisha na kuimarisha shughuli hiyo ya utafiti ikiwemo kuwafikia kikamilifu wakulima za zao hilo.

Pia ametumi nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa taasisi hiyo kwa kazi mzuri ya utafiti  inayoendelea kufanyika kwani ndio moyo wa kilimo nchini.

“Ninyi msipofanya kazi yenu vizuri sekta ya kilimo haitaendelea, haitaweza kukuwa hivyo hatutaweza kufikia malengo tuliyojiwekewa kama nchi ya kukuza uchumi.”amesema Magala.

Mkurugenzi Mkuu wa Tari Dk. Thomas Bwana amesema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa na umahiri mkubwa katika utendaji kazi wake kwani inafanya tafiti inayokwenda kutatua changamoto za watu wakiwemo wakulima.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred  amesisitiza suala zima la kuhudumia wakulima kikamilifu ili kuleta teknolojia  inayoanzia shambani na mwisho wa siku kuleta uzalishaji wenye tija.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button