NACTEVET yaridhishwa maandalizi mashindano ya ujuzi

TANGA: MAANDALIZI ya Mashindano ya Ujuzi Kitaifa (WorldSkills Tanzania 2026) yanayotarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara mkoani Tanga yamefikia hatua nzuri na kuridhisha.

​Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Mwajuma Lingwanda, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu  hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya kitaifa.

​Akizungumzia utayari wa tukio hilo, Dk. Lingwanda amesema kuwa washiriki, waamuzi (judges), pamoja na wataalamu wa fani mbalimbali zinazoshindanishwa, wapo tayari .

​Aidha, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wa mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani kufika katika viwanja hivyo ili kushuhudia kwa karibu umahiri na ufundi stadi unaooneshwa na vijana wa Kitanzania katika nyanja mbalimbali.

​Dk. Lingwanda amebainisha kuwa washindi wa kwanza katika kila fani watapata fursa ya kipekee ya kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Ujuzi ya Afrika (WorldSkills Africa) yatakayofanyika hivi karibuni

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button