Wanne wapandikizwa figo Mloganzila

DAR ES SALAAM; Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila imepandikiza figo wagonjwa wanne katika kambi maalumu iliyofanyika Agosti 16 hadi 19, mwaka huu, huku jumla ya wagonjwa 28 wakifanyiwa huduma hiyo tangu kuanza Aprili 2023.
Akizungumza baada ya kutembelea wagonjwa hao, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji MNH-Mloganzila, Dk Godloven Mfuko, amesema wagonjwa hao walipokea figo kutoka kwa ndugu zao na wengi wao walikuwa wamefikia siku ya nane baada ya upasuaji, hivyo kuwa tayari kuruhusiwa.
Amesema katika kambi hiyo pia wagonjwa 38 walipata huduma , ambapo 37 walifanyiwa upasuaji wa kutengeneza mishipa ya damu kwa ajili ya kuchujia damu na mmoja aliwekewa kifaa maalumu.
Dk Mfuko amesema tangu kuanza kwa huduma ya kutengeneza mishipa ya damu kwa wagonjwa wanaosafisha figo mwaka 2024, jumla ya wagonjwa 208 wamenufaika na huduma hiyo.
Amesema huduma hizo ni sehemu ya jitihada za hospitali hiyo kuhakikisha wagonjwa wenye matatizo ya figo wanapata huduma za kibingwa nchini, huku akishukuru serikali kwa uwekezaji katika vifaatiba, miundombinu na mafunzo ya wataalamu.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, Figo na Afya ya Uzazi kwa Wanaume, Dk David Mgaya, amesema mchangiaji wa figo hufanyiwa upasuaji kwa matundu madogo ambapo upasuaji huchukua chini ya saa mbili.
“Faida ya aina hii ya upasuaji ni kupunguza maumivu, muda wa kupona na ukubwa wa kovu ikilinganishwa na upasuaji wa kawaida wa kufungua tumbo.
Dk Mgaya amesema kabla ya mchangiaji kufanyiwa upasuaji, wataalamu huchunguza mishipa ya damu ya figo ili kubaini idadi na muundo wake na kuhakikisha figo inayotolewa inaweza kutumika salama kwa mpokeaji.
“Baada ya figo kutolewa, hufanyiwa maandalizi maalumu yanayojulikana kama table surgery, ambapo wataalamu huandaa figo na mishipa yake kabla ya kuiunganisha kwa mpokeaji.
Alisema endapo figo ina mishipa zaidi ya mmoja inayosambaza damu, wataalamu hufanya reconstruction ili kuiandaa kwa ajili ya kupandikizwa na kuhakikisha inapata mtiririko mzuri wa damu.
Naye Daktari Bingwa na Mhadhiri wa Magonjwa ya Figo MNH-Mloganzila Dk Anthony Gyunda amesema takribani asilimia 10 ya watu duniani wana matatizo ya figo katika hatua mbalimbali, huku ugonjwa huo ukiwa na hatua tano.
Amesema mgonjwa anapofikia hatua ya mwisho, figo hushindwa kufanya kazi na huhitaji msaada wa kitabibu kupitia dialysis au upandikizaji figo, ambao ndio tiba ya kudumu kwa wagonjwa wanaokidhi vigezo.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com