Rais Samia awakumbuka wahitaji

RAIS Dkt Samia Suluhu ametoa zawadi mbalimbali ikiwemo vyakula kwa watu wenye uhitaji zaidi ya 500 wilaya Korogwe kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid.
Mufti wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeir amegawa zawadi hizo kwa niaba ya Rais wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali.
Akizungumzia kabla ya zoezi hilo Mufti Zubeir amewataka watanzania kumuombea Rais Samia ili aweze kuongoza nchini kwa usalama na amani.
“Leo nimekuja kushiriki Iftar lakini pamoja na ugawaji wa zawadi mbalimbali kwa makundi ya watu wenye uhitaji, niwaombe ndugu zangu tumuombe Dua Rais wetu aweze kuongoza nchi kwa salama na amani.



