ITALIA: BEKI wa Italia na klabu ya Arsenal, Riccardo Calafiori alilzimika kutolewa nje kutokana na majeraha katika mchezo wa ‘Nations League’ uliopigwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Ufaransa, mchezo ulioisha kwa Italia kushinda mabao 3-1.
Beki huyo aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 42 majira ya kiangazi huko Emirates, alipata jeraha la kifundo cha mguu baada ya mshambuliaji wa klabu ya PSG, Ousmane Dembele kumuangukia beki huyo kufuatia kugongana na Alessandro Bastoni.
Calafiori alicheza zaidi ya saa moja ya pambano hilo kwenye uwanja wa Parc des Princes lakini aliondolewa na madaktari muda mfupi baada ya tukio hilo huku Italia wakiwa mbele kwa mabao 3-1.
Pengine tukio hilo huenda likampa wasiwasi kocha wa Arsenal, Mikel Arteta hofu ikiwa mwendelezo wa majeruhi kwa wachezaji wapya wa kikosi chicho. Ikumbukwe kiungo mpya wa klabu hiyo Mikel Merino naye ameumia akiwa hajacheza mchezo wowote.
SOMA: Arsenal yaitangulia Juve kuwania saini ya Calafiori
Pia mshambuliaji Gabriel Jesus naye ameumia, wasiwasi mwingine kuelekea mchezo wa Jumamosi ijayo ambapo Arsenal itakuwa Tottenham Stadium dhidi ya Spurs, hukuu ikikosa Declan Rice ambaye anatumikia kadi nyekundu.