PSG yaongoza mbio kumsajili Mohamed Salah

Fowadi wa Liverpool na Misri, Mohamed Salah.

TETESI za usajili barani Ulaya zinasema Paris Saint-Germain inaongoza mbio kumsajili fowadi wa Misri Mohamed Salah na itajaribu kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye mkataba wake Liverpool unamalizika mwisho wa msimu huu, asaini dili la miaka mitatu.(Sun)

Liverpool inamvutia kasi fowadi wa Borussia Dortmund, Karim Adeyemi awe mbadala wa Salah, na ipo tayari kuwasilisha ombi la pauni milioni 41 kumsajili mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 22. (Bild – in German)

SOMA: Kishindo cha siku ya mwisho dirisha la usajili Ulaya

Advertisement

Makocha Thomas Tuchel na Massimiliano Allegri wanaongoza katika orodha kuchukua mikoba Manchester United wakati timu hiyo inafikiria kumfuta kazi Erik ten Hag. (Teamtalk)

Manchester United inaandaa ombi la kumsajili winga wa kituruki anayekiwasha klabu ya Benfica anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 34, Kerem Akturkoglu, 25. (Fichajes – in Spanish)

Chelsea bado inamfukuzia fowadi wa Colombia, Jhon Duran, lakini Aston Villa inataka zaidi ya pauni milioni 80 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Teamtalk)

Barcelona na Juventus zinafuatilia hali ya winga wa Argentina, Alejandro Garnacho, 20, huku Manchester United ikiaminika kumweka mchezaji huyo kuwa na thamani ya pauni mil 50. (Sun)