ACT yasisitiza amani kupitia mazungumzo

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesisitiza umuhimu wa kulinda na kuendeleza amani ya Tanzania kwa kutumia mazungumzo na maridhiano, kikieleza kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa chanzo cha migogoro bali fursa ya kutafuta mwafaka kwa maslahi ya taifa.

Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa ACT Wazalendo Taifa, Salim Bimani, amesema uzoefu wa mazungumzo ya maridhiano Zanzibar yaliyofanyika kwa miezi minane baada ya uchaguzi umeonyesha kuwa hata tofauti kubwa zinaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Amesema hatua ya kufikiwa kwa makubaliano ya kisiasa ni ushahidi kuwa mazungumzo ndiyo njia bora ya kujenga umoja, amani na kuimarisha utulivu nchini.

“Tunatoa wito kwa Watanzania wote kulinda amani kwa kukaa mezani na kuzungumza. Tofauti zipo, lakini jambo la msingi ni kufikia mwafaka kwa mazungumzo,” amesema.

Bimani amesisitiza kuwa makubaliano yanapaswa kutekelezwa kikamilifu ili kuimarisha imani na kudumisha maridhiano ya kisiasa.

Aidha, amewataka wadau wote wa siasa, hususan vyama vya upinzani, kuwa na mtazamo mpana unaotanguliza maslahi ya taifa, akieleza kuwa mazungumzo endelevu ndiyo yatakayowezesha nchi kuendelea kuwa na amani, umoja na utulivu.

Ameongeza kuwa kukutana na kujadiliana mara kwa mara kutasaidia kujenga utamaduni wa maridhiano na kuondoa tofauti zinazoweza kuhatarisha mshikamano wa Watanzania.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button