Dk Kijaji atembelea shule, asikiliza kero za wananchi

KAGERA: WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Ashatu Kijaji ameweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Msingi Kihumulo iliyogharimu Sh milioni 330.7 na kutembelea mradi wa ujenzi wa Bwalo la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kagera pamoja sambamba na kusikiliza kero za wananchi.
DK Kijaji amewahakikishi wananchi wa Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kuwa serikali kupitia itaendelea kupunguza changamoto ya wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu huku akidai kuwa serikali inaendelea kuweka nguvu katika ujenzi wa vyuo vya ufundi standi.
Akizungumza na wananchi wa Mji Mdogo wa Mtukula kupitia ziara yake, Dk Kijaji amesema vipo baadhi ya vijiji ambavyo watoto wengi wanasitisha ndoto zao kutokana na umbali na ndio maana serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu.

Amesema serikali itaendelea kuwekeza katika vyuo vya ufundi stadi kwa ajili ya kutoa ujuzi wa kiufundi na kuandaa vijana wengi zaidi kujiajili ambapo wilaya ya Missenyi wataendelea kunufaika na mpango wa ujenzi wa chuo hicho.
Aidha, Waziri Kijaji amezitaka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kuhakikisha shule hiyo pamoja na nyingine zinaendeshwa kwa ufanisi na elimu inatolewa kwa ukamilifu ili kufikia lengo la serikali la kutoa elimu bora kwa watoto wote nchini.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, msimamizi wa ujenzi, Mutalemwa Makwabe, amesema shule hiyo itakuwa mkombozi kwa watoto wa Kata ya Mtukula kwa kuwawezesha kupata elimu bora katika mazingira rafiki na kuongeza kwa kusema shule hiyo itarahisisha upatikanaji wa elimu kwa watoto wengi wa eneo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Misenyi Frorent Kyombo, amesema zaidi ya Sh bilioni 1.2 zimeelekezwa katika kuboresha sekta ya elimu wilayani humo ambapo baadhi ya vijiji vimepata miradi kujengewa shule mpya na watoto kupata elimu karibu.




I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. https://www.work27.info