Kihongosi: Vijana ni walinzi wa nchi yetu

IRINGA: Katibu NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesisitiza kuwa vijana ndio walinda nchi, hivyo wanatakiwa kuilinda amani ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya taifa na familia zao.

Kihongosi ameyasema hayo leo Agosti 10, 2026 wakati akitoa mada kwenye Mafunzo ya Uongozi wa Seneti za Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo Ihemi mkoani Iringa.

Pia, ametumia jukwaa hilo kukemea lugha chafu zinazotolewa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika mitandao ya kijamii na kuwasihi vijana kuwa mstari wa mbele kumtetea Rais na wasikae kimya.

Aidha, ametoa wito kwa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndani na nje ya Tanzania kulipa ada ya uanachama akieleza uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unatokana na wanachama kulipia ada.




