Wafukua kaburi, wadaiwa kuchukua mabaki ya mwili

KATAVI; Familia ya Zacharia Anthony wa Mtaa wa Nsemulwa, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, imekumbwa na sintofahamu baada ya kaburi la ndugu yao aliyezikwa mwaka 2012 kufukuliwa na watu wasiojulikana, huku mabaki ya mwili yakidaiwa kuchukuliwa.

Familia iligundua tukio hilo walipokwenda makaburini kwa ajili ya kusafisha na kuandaa ujenzi wa makaburi yao.

Mama mzazi wa marehemu, Adela Zacharia, amesema kitendo hicho kimemuongezea maumivu na kujiuliza sababu ya kufukulia kaburi la mwanaye.

“Nashangaa ni kitu gani ambacho kimesababisha mpaka kuja kufukua tena kaburi la mwanangu, na mbaya zaidi wamebeba hadi mifupa ya mwanangu, mpaka sasa najiuliza, kwa nini?” Amehoji Adela.

Ndugu wa marehemu, Philipo Zacharia, amesema familia ilikuta kaburi limefukuliwa, mifupa ikiwa haipo na sanda ikiwa imeachwa pembeni, huku wakiamini tukio hilo lilifanyika siku chache kabla ya wao kufika.

“Tulijipanga kama familia kuja kujengea makaburi, likiwemo hili, na kumalizia kuweka marumaru. Tulipofika kwa ajili ya kusafisha kwanza ndipo tukakuta hali tofauti. Kaburi limefukuliwa na wamebeba mpaka mifupa ya marehemu, huku sanda aliyokuwa amevishwa ikiwa imewekwa pembeni,” amesema Philipo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nsemulwa, Emili Robert, amethibitisha tukio hilo na kusema lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Agosti 8, akisema eneo hilo limekuwa likiripotiwa matukio ya uhalifu, baadhi yakihusishwa na imani za kishirikina.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button