Taasisi yasaidia huduma upatikanaji chakula shuleni

GEITA; Taasisi  ya Mapung’o Foundation iliyopo mkoani Geita imetoa msaada wa gunia 75 za mahindi ya chakula katika Shule ya Sekondari Nyakagwe, ili kuunga mkono upatikanaji wa chakula shuleni.

Msaada huo unalenga kufanikisha utekelezaji wa sera ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni wakati wa masomo na kutengeneza mazingira rafiki ya kujifunza.

Mratibu wa Mapung’o Foundation, Marco Victor amekabidhi msaada huo leo kwa niaba ya taasisi ambapo msaada huo uliambatana na boksi 17 za karatasi.

Ofisa Elimu wa Kata ya Butobela, Andiyo Otyeno amesema kuwa msaada wa chakula shuleni hapo utachochea maendeleo ya elimu kwani wanafunzi watapata muda wa kutosha wa kusoma.

Amesema baada ya kupata uhakika wa chakula, wameweka mpango maalumu wa kambi za masomo kwa wanafunzi wa kidato cha pili na kidato cha nne ili wajiandae na mtihani wa taifa.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyakagwe, George Edward amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 452 na kwamba msaada uliotolewa utasaidia siyo tu wanafunzi wa bweni,  lakini pia wanafunzi wa kutwa ambao watapata uhakika wa upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni bila usumbufu.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button