Ushirikiano Takukuru, NAOT waokoa Sh Bil 19

ARUSHA; TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema ushirikiano wake na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) umewezesha kuokoa takribani Sh bilioni 19 zilizokuwa katika hatari ya kupotea kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma katika sekta ya manunuzi.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Neema Mwakalyelye, ametoa kauli hiyo leo jijini Arusha wakati wa Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Kikosi Kazi cha Kupambana na Rushwa na Ufujaji wa Fedha, ulioandaliwa na NAOT.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2023 hadi 2026, jumla ya majalada 470 ya uchunguzi yalifanyiwa ukaguzi maalumu wa kiuchunguzi, huku ripoti 130 za ukaguzi zikitumika katika kesi au taratibu za mahakamani na kesi 76 zilihitimishwa kwa mafanikio kutokana na mchango wa taarifa za CAG, huku kesi 67 zikihusisha urejeshaji wa fedha
“Ushirikiano huu umeonesha wazi kuwa taarifa za ukaguzi zinapotumika kwa wakati na kwa ufanisi, zinaweza kusaidia hatua za kisheria na kurejesha fedha za umma,” amesema.
Amesema eneo la manunuzi lina vihatarishi vya rushwa, udanganyifu na upangaji wa zabuni, akibainisha kuwa manunuzi ya umma yanachangia zaidi ya asilimia 70 ya matumizi ya serikali.
Kwa upande wake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amezitaka taasisi zinazohusika na manunuzi ya umma, ukusanyaji wa kodi, mapambano dhidi ya rushwa na utakatishaji wa fedha kuimarisha ushirikiano, ili kuziba mianya inayotumiwa kuficha umiliki halisi wa kampuni na kutekeleza uhalifu wa kifedha.
Kichere amesema ushirikiano huo ni muhimu kuhakikisha watu wanaoficha umiliki wa kampuni hawatumii mianya iliyopo kati ya taasisi za serikali kutekeleza vitendo vya kifedha visivyo halali.
Amesema ushirikiano huo unapaswa kuhusisha mamlaka za manunuzi, wizara na taasisi za serikali, mamlaka za mapato, taasisi za kupambana na rushwa, vitengo vya ujasusi wa fedha, vyombo vya sheria na taasisi kuu za ukaguzi.
“Taasisi Kuu za Ukaguzi zitumie taarifa mlizonazo kuhusu wamiliki halisi wa kampuni, zitoe mapendekezo madhubuti ya ukaguzi na hatua zinazoweza kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi,” amesema Kichere




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com