Kagera yapokea vifaa kilimo cha umwagiliaji

KAGERA: Mkoa wa Kagera, kupitia Tume ya Umwagiliaji umepokea vifaa vya umwagiliaji kutoka Wizara ya Kilimo, vyenye thamani ya Sh bilioni 1.2 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kuendelea na uzalishaji wa mazao bila kutegemea mvua.
Lengo la hatua hiyo ni kuongeza uzalishaji wa kilimo kwa kuwawezesha wakulima kutumia teknolojia ya umwagiliaji na hivyo kupunguza utegemezi wa mvua katika shughuli zao za kilimo na Kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo kwa vikundi 146 vya wakulima,wa mkoa wa Kagera huku akisisitiza umuhimu wa kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao
Amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kuongeza uhakika wa uzalishaji wa chakula kwa ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla kwa misimu mbalimbali kwa ukanda wa mkoa wa Kagera na Kanda ya Ziwa.

Amezitaka Mamulaka za serikali za mitaa kuhakikisha zinasimamia vikundi hivyo na kuvisajili kisheria na kutoa taarifa za uzalishaji baada ya muda mfupi ,kutoa mafunzo namna ya kutumia vifaaa hivyo Kwa weledi na kutunga sheria ndogo ndogo kwa vikundi vyenye nia ovu ya kukodisha vifaa hivyo au kuviuza kinyume na matakwa
Taarifa iliyotolewa na Mhandisi wa tume ya umwagiliaji mkoani Kagera Said Mbiru alisema kuwa vikundi vilivyopokea vifaa ni 146 vyenye uwezo wa wakulima 2193
Alisema vifaa hivyo vinauwezo wa kurusha maji Lita 80,000 kwa saa na kumwagilia hekari 28 kwa saa.

Alisema hiyo ni awamu ya kwanza Kwa wakulima wadogo kupata vifaa hivyo na awamu ya pili itahusisha wakulima wengi zaidi kwenye vikundi vyao .
Katibu wa itikadi na uenezi chama Cha mapinduzi CCM Hamimu Mahamud amesema ilani ya chama Cha mapinduzi ya mwaka 2025-2030 inasema kuwa serikali itaendelea kuwajali wananchi wake wakiwemo wakulima kwa kuhamasisha kwa vitendo kilimo cha umwagiliaji bila kusubiri mvua.

Amesema ni vyema wakulima wakashikama na kujiuga kwenye vikundi ili wapate kuhudumiwa kwa pamoja kama kupewa mitaji,dhana za kilimo pembejeo na mbolea na kwa njia hiyo wakulima wanakuwa wamenufaika na utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi.
Mwakilishi wa vikundi vya wakulima Recho Chacha kutoka kikundi Cha Kinyerere Kagya Amesema serikali imefanya jambo kubwa kwa wakati uliopo kutokana na majira kubadilika badilika na kukosekana kwa mvua za uhakika.
Amewasilisha ombi la wakulima la kupewa trecta ndogo za kilimo ili kupiga hatua kubwa za kuingia katika wakulima wakubwa na kudai kuwa jembe la mkono linachosha na matokeo yanakuwa kidogo .



