Mwenge wazindua barabara ya Kajai–Bwanjai

KAGERA: Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026 zimezindua Barabara ya Kajai–Bwanjai yenye urefu wa kilomita moja iliyojengwa kwa kiwango cha lami, inayowaunganisha wananchi wa Wilaya za Bukoba na Missenyi katika kupata huduma katika Hospitali Teule ya Mugana wilayani Missenyi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amepongeza namna Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ulivyotekeleza mradi huo kwa viwango, akisema umeleta manufaa kwa wananchi wengi wanaotumia barabara hiyo.

Aidha, mmoja wa wananchi wa eneo hilo amejitolea kuweka taa za barabarani, jambo ambalo limekuwa kivutio kwa wananchi na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Kutokana na hatua hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amemkabidhi mwananchi huyo hati ya pongezi na kuwataka wananchi wengine kuendelea kuwa wazalendo na kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Missenyi, Mhandisi Sperius Kikarangirwa, amesema mradi huo umegharimu zaidi ya Sh milioni 400.

Amesema mradi huo umekamilika na sasa wananchi wananufaika na barabara hiyo kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo, huku baadhi yao wakianza kujenga majengo kandokando ya barabara hiyo.
Baadhi ya wananchi wanaotumia barabara hiyo wameishukuru Serikali kwa kutatua changamoto iliyodumu kwa muda mrefu, wakisema awali magari yalikuwa yakikwama wakati wa mvua na kusababisha usumbufu, hasa kwa wagonjwa waliokuwa wakielekea Hospitali Teule ya Mugana.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com