Ngassa, Fikirini wang’ara Tuzo Ligi Kuu

DAR ES SALAAM; KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Dodoma Jiji, Berno Ngassa amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2026/27, huku Fikirini Elias wa Coastal Union akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imesema Ngassa alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Maabad Maabad wa Coastal Union na Anuar Jabir wa Polisi Tanzania, alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

“Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo miwili ambayo  ilicheza mwezi huo na kushinda yote, huku nyota huyo akifunga bao moja na kuhusika na lingine moja.

“Kwa upande wa Fikirini aliyeingia fainali na Steve Barker wa Simba na Vicent Mashami wa Dodoma Jiji, aliiongoza Coastal Union kushinda michezo yote miwili iliyocheza mwezi huo na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 11 kwenye msimamo wa ligi,” imesema taarifa hiyo.

Pia taarifa imesema kamati imeteua magoli matatu bora, ambayo yatapigiwa kura na mashabiki ili kupata goli bora la mwezi Septemba. Magoli hayo ni  Haroun Lyawatwa (Mashujaa v Singida BS), Anuary Jabir (Polisi V Mbeya City) na Mohamed Damaro (Singida BS v Namungo).

“Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Ramadhan Kalanje wa KMC kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba wa Ligi ya Championship, akiwashinda Abiud Mtambuku wa Mbeya Kwanza na kipa Haroun Mandanda wa Rhino Rangers,” imesema taarifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya bodi upande wa Kocha Bora wa ligi hiyo, kamati ilimchagua Mohamed Muya wa KMC aliyeiongoza timu yake kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mwezi huo akiwashinda Salvatory Edward wa Rhino

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button