Prof Mkumbo akaribisha wawekezaji kutoka Uholanzi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uholanzi kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, hususan katika sekta za uzalishaji viwandani, usindikaji wa mazao na uongezaji thamani.
Akizungumza jijini The Hague, Uholanzi, Prof. Mkumbo amesema nafasi ya kimkakati ya Tanzania kijiografia, pamoja na miundombinu na masoko yanayozunguka nchi, vinaifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha uzalishaji, biashara na usambazaji wa bidhaa katika masoko ya Afrika na kwingineko.

Amesema Serikali inaendelea kuweka msukumo katika uwekezaji unaolenga kuongeza thamani ya mazao na rasilimali zinazopatikana nchini badala ya kusafirisha malighafi, hatua ambayo inalenga kuimarisha sekta ya viwanda, kuongeza ajira, kupanua biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Prof. Mkumbo ameeleza pia kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, ikiwemo kurahisisha huduma kwa wawekezaji na kuweka mazingira yanayowezesha sekta binafsi kuwa injini muhimu ya maendeleo ya Taifa.

Aidha, amesisitiza kuwa amani, utulivu wa kisiasa, rasilimali nyingi na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini vinaendelea kuifanya nchi kuwa moja ya maeneo yenye fursa kubwa kwa wawekezaji wanaotafuta masoko ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya uhamasishaji wa uwekezaji barani Ulaya, iliyoanza Helsinki, Finland tarehe 28 Septemba 2026, na kuendelea nchini Italia kabla ya kufika Uholanzi. Ziara hiyo pia ni sehemu ya maandalizi kuelekea Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam mwaka 2027.
Kupitia ziara hiyo, Tanzania inalenga kuimarisha mahusiano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ulaya, kuvutia mitaji mipya na teknolojia, pamoja na kubadilisha majadiliano ya uwekezaji kuwa miradi halisi inayotekelezwa nchini.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com