Zuchu akubali yaishe
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Zuhura Othuman ‘Zuchu’ ameomba radhi kwa Watanzania kufuatia maneno aliyotumia kwenye onesho lake la ‘full moon’ alilolifanya wiki moja iliyopita Zanzibar.
Zuchu ameomba radhi kupitia taarifa aliyoitoa jana jioni kwenye mitandao ya kijamii.
“Najua kuwa maneno yalileta sintofahamu kwa wengi wenu na kuleta maana hasi kwa jamii na mashabiki zangu kwa ujumla, nia yangu ilikuwa ni kuleta burudani njema na furaha kwa mashabiki wangu wote,”
Zuchu amesema halikuwa lengo lake kupotosha, kumong’onyoa maadili au kuleta taharuki, hata hivyo Zuchu ameahidi kufanya kazi na timu yake ili kuhakikisha matukio kama hayo hatokei tena.
Akiwa visiwani humo katika onesho lake, Zuchu alitumia maneno yaliyotafsiriwa kuwa machafu yaliyopelekea kuleta taharuki kwa baadhi ya watu mitandaoni.



