Msuva azungumzia ndoto Kombe la Dunia

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Taifa Stars, Simon Msuva, amesema bado ana ndoto ya kuichezea Tanzania katika fainali za Kombe la Dunia kabla ya kustaafu soka, huku akiwataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono timu hiyo katika safari yake ya kimataifa.

Msuva, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Al-Talaba ya Iraq, amesema licha ya kuwa kila taifa lina mipango yake kuelekea fainali za AFCON, yeye bado ana malengo makubwa akiwa na timu ya taifa.

“Kwa upande wangu kama mchezaji, plan yangu ni kucheza siku moja kabla sijastaafu. Pia natamani siku moja kucheza fainali na siyo tu kufika fainali,” amesema Msuva.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa ndani ya Taifa Stars, akiwa pia sehemu ya kikosi kilichofuzu AFCON 2025 baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa Tanzania wa 1-0 dhidi ya Guinea kwenye mchezo wa mwisho wa kufuzu.

Akizungumzia nafasi ya Tanzania kufanya vizuri, Msuva amesema bado kuna nafasi kubwa ya kufikia malengo, lakini amesisitiza umuhimu wa kupata sapoti kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Msuva mwenye umri wa miaka 32 pia amesema hana mpango wa kustaafu kwa sasa, akieleza kuwa bado anajiona akiwa katika hali nzuri ya kimwili na kiushindani.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button