GGML yaunga mkono uhabarishaji wenye tija Geita

GEITA: KAMPUNI ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) imeweka wazi kuwa ipo tayari kufanya kazi na vyombo vyote vya habari ili kuunga mkono uhabarishaji wenye tija kwa maslahi ya umma.

Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma GGML, Stephen Mhando amesema hayo katika warsha maalum ya waandishi mkoani Geita iliyoandaliwa na GGML.

Amesema GGML kupitia kitengo cha mahusiano kwa umma imejizatiti kuendeleza ushirikiano ili kufanikisha wanahabari wote bila ubaguzi wanapata taarifa sahihi kuhusu shughuli zake.

Mhando amesema matamanio ya GGML ni kuona jamii inapata taarifa sahihi, kwa wakati sahihi na kutoka vyanzo sahihi kuhusu uwekezaji wa GGML pamoja na miradi inayotekelezwa na serikali.

Amesema uhabarishaji wenye tija utapunguza ama kuondoa kabisa migogoro isiyo ya lazima baina ya wawekezaji na jamii, wawekezaji na serikali au jamii na serikali kuhusu miradi ya maendeleo.

Naye Mwezeshaji katika warsha hiyo, Mwandishi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Sammy Awami amesisitiza waandishi wa habari kuzingatia misingi ya kitaaluma.

Amesema uhabarishaji wenye tija ni ule unaozalisha habari zenye mvuto kwa hadhira pasipo kukiuka misingi ya kitaaluma kwa kuhusisha vyanzo sahihi pasipo kuegemea upande mmoja.

Amesema mwandishi anayezingatia taaluma yake na kutekeleza wajibu wake bila upendeleo ana nafasi kubwa ya kuzalisha taarifa zenye thamani na zinazoleta mapinduzi chanya katika jamii.

Awali akifungua warsha hiyo Makamu wa rais wa AngloGold Ashanti inayomiliki GGML, Simon Shayo amesema wanathamini vyombo vya habari kwani ni wadau muhimu katika utendaji wao.

Shayo amesema maono ya GGML ni kushirikiana na taasisi zote za binafsi na serikali ambapo taarifa sahihi zitasaidia kuchochea ushirikiano wenye tija katika shughuli za uwekezaji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button