Hatma ya Ten Hag kuamuliwa leo

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag.

TETESI za usajili barani Ulaya zinasema hatma ya kocha Erik ten Hag katika klabu ya Manchester United itaamuliwa wakati wa mkutano wa timu hiyo leo huku msaidizi wake, Ruud van Nistelrooy akipewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi kama kocha wa muda iwapo mabadiliko yatafanyika.(Guardian)

Manchester United inapanga mjerumani Thomas Tuchel awe mbadala wa Ten Hag. (Manchester Evening News)

SOMA: Simone Inzaghi ‘kumrithi’ Ten Hag

Advertisement

Ten Hag raia wa Uholanzi bado ana imani bado anahitajika kwa mabosi wa Manchester United kuelekea mapumziko ya kalenda ya kimataifa.(ESPN)

Liverpool ina nia kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na Misri, Omar Marmoush, 25.

Nottingham Forest na Aston Villa zilitaka kumsajili Marmoush majira yaliyopita ya kiangazi. (Sky Germany – in German)

Manchester City inafikiria uhamisho wa kiungo mhispania wa Real Sociedad, 25, Martin Zubimendi Januari 2025 kuchukua nafasi ya majeruhi Rodri. (Relevo – in Spanish)

Barcelona inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David, 24. (Todofichajes – in Spanish)