TETESI za usajili barani Ulaya zinasema Manchester United ina nia kumuajiri kocha wa Inter, Simone Inzaghi iwapo klabu hiyo ya Old Trafford itaachana na Erik ten Hag.
Pia Man United inamfikiria kocha wa zamani wa England, Gareth Southgate. (Daily Star)
Manchester City inaweza kuvamia kambi ya Real Sociedad kwa ajili ya kumsajili Martin Zubimendi Januari,2025 wakati ikiimarisha msako wa mbadala wa nyota wake majeruhi, Rodri.
Liverpool pia inaweza kufufua mpango wake wa kumsajili Rodri.(Football Insider)
SOMA: Man United yahangaika kusaka mbadala wa Casemiro
Arsenal pia inasaka saini ya Zubimendi, lakini inaamini anashikilia msimamo wa kuhamia Real Madrid. (TBR Football)
Hata kama Zubimendi hatajiunga na Emirates, Arsenal inatarajiwa kusajili kiungo mpya majira ya kiangazi 2025.(CaughtOffside)
Man Utd na Livrpool zote mbili zinaitaka saini ya fowadi wa Eintracht Frankfurt, Omar Marmoush, ambaye ana mabao 6 na pasi za mabao 3 katika michezo 5 ya Ligi Kuu Ujerumani -Bundesliga msimu huu. (BILD – Germany)